Tanzania yashika nafasi ya nne barani Afrika kwa usalama wa anga
2023-10-31 08:27:19| cri

Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amesema jana kuwa Tanzania imeshika nafasi ya nne kwa usalama wa anga barani Afrika baada ya Nigeria, Kenya, na Cote d'Ivoire.

Bw. Majaliwa amesema, Tanzania ilipata asilimia 86.7 katika tathmini iliyofanywa mwezi wa Mei na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro, Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, na Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar.

Amesema kutokana na kuongezeka kwa usalama wa anga, Tanzania imekuwa ikirekodi ongezeko la abiria wanaotumia viwanja vyake vya ndege, na kuuongeza kuwa, idadi ya abiria iliongezeka kutoka 1,662,452 mwaka 2003 hadi 4,614,380 kufikia mwezi Septemba mwaka 2023.