Kampuni za simu za Kenya zashirikiana na kampuni ya China kuzindua kiwanda cha simu janja
2023-10-31 08:24:42| CRI

Rais wa Kenya William Ruto amezindua kiwanda cha kutengeneza simu kwa ushirikiano kati ya kampuni za simu za Kenya Safaricom na Jamii Telecom, pamoja na Kampuni ya simu ya China Shenzhen TeleOne Technology.

Rais Ruto amesema Kiwanda cha Kutengezeza Simu ya Afrika Mashariki (EADAK) kilichoko katika mji wa Athi River, kitatengeneza simu milioni tatu kila mwaka, na kuongeza kuwa Kenya haitafaidika tu na nafasi za ajira bali pia itanufaishwa kwa bidhaa zenye bei nafuu zaidi.

Vilevile Rais Ruto amesifu ushirikiano kati ya Kenya na China kwa kuwa kiwanda hicho kitaimarisha hadhi ya Kenya ikiwa nchi yenye nguvu ya uchumi wa kidijitali na uongozi wa teknolojia na uvumbuzi.