UNECA yasema Afrika yatakiwa kutimiza usalama wa chakula na nishati ili kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu
2023-10-31 08:26:25| CRI

Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imesema, kutimiza usalama wa chakula na uhamishaji wa nishati ni muhimu katika kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) barani Afrika.

Katika taarifa yake, Tume hiyo imesema, kutokana na hali tete ya uchumi wa dunia iliyosababishwa na janga la COVID-19 na athari za vita kati ya Russia na Ukraine katika bei ya chakula na nishati, kutimiza usalama wa chakula na uhamishaji wa nishati ni jambo muhimu kwa nchi za Afrika, hususan kanda za Kaskazini na Magharibi mwa bara hilo.

Tume hiyo imesema, usalama wa chakula na nishati katika eneo la Kaskazini na Magharibi mwa Afrika vimekabiliwa na athari kubwa, huku takwimu zikionyesha kuwa kati ya mwaka 2019 na 2022, karibu watu milioni 25 zaidi walikabiliwa na lishe duni katika maeneo hayo.