Baraza la Kumi la Xiangshan lafungwa hapa Beijing
2023-11-01 08:42:44| cri


 

Baraza la Kumi la Xiangshan limefungwa jana hapa Beijing.

Baraza hilo limehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1800 wakiwemo mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 19, makamanda wakuu wa majeshi ya ulinzi kutoka nchi 14, wajumbe wa mashirika 6 ya kimataifa, wataalamu na wasomi, na wachunguzi wa nchi mbalimbali, ambao walijadiliana kuhusu “Usalama wa Pamoja na Amani ya Kudumu”.

Baraza la Xiangshan limekuwa jukwaa muhimu la kutoa pendekezo la usalama wa dunia na kuhimiza ushirikiano wa usalama wa kikanda.