Wanajeshi wa Israel waingia kaskazini magharibi mwa mji wa Gaza
2023-11-01 08:36:37| cri

Idara ya mambo ya ndani ya Ukanda wa Gaza ya Palestina imesema, wanajeshi wa vifaru vya Israel wameingia katika wilaya ya Karama, kaskazini magharibi mwa Mji wa Gaza jana.

Wakati huohuo, wapiganaji wa kundi la Houthi la nchini Yemen wamesema wameanza mashambulio ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel hapo jana ili kulipiza kisasi operesheni za kijeshi za Israel dhidi ya kundi la Hamas.

Idara ya afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imesema kuwa, operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza zimesababisha vifo vya watu 8,525 na kujeruhi zaidi ya watu 21,000.