Benki Kuu ya Tanzania yasema ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo uko katika mwelekeo sahihi
2023-11-01 08:39:32| CRI

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuwa, ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo uko katika mwelekeo sahihi kutimiza ukuaji wa asilimia 5.3 katika mwaka 2023.

Katika taarifa yake, Benki hiyo imesema ukuaji katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka huu umekuwa wa kuridhisha, ukifikia asilimia 5.4 na 5.2.

Taarifa hiyo pia imesema, uchumi wa visiwani Zanzibar umekua kwa asilimia 6.2 katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, na unatarajiwa kufikia lengo la ukuaji la mwaka la asilimia 7.1.