Washauri wa kisiasa wa China wajadili ulinzi wa mazingira na ujenzi wa China Bora
2023-11-01 08:37:56| CRI

Washauri wa kisiasa wa China wamebadilishana maoni kuhusu kuimarisha ulinzi wa mazingira na kuboresha ujenzi wa China Bora.

Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), Wang Huning, amehudhuria kikao cha nne cha Kamati ya Kudumu ya awamu ya 14 ya CPPCC.