Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo
2023-11-01 10:44:41| cri

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewahakikishia wakulima wa Tanzania dhamira yake ya kuwawezesha katika kuhimiza mabadiliko na kufanya kilimo chao kuwa cha kibiashara.

Ofisa mwandamizi wa Benki hiyo Bw. Edson Rwechungura amesema mjini Dar es Salaam kuwa mbali na kutoa mikopo, lengo la benki hiyo ni kutoa mafunzo, ushauri, na utafiti ili kuongeza uwezo wa kuwashauri wakulima kuwa na kilimo chenye tija.

Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango wa TADB, Bw. David Waziri amesema benki hiyo inatoa zaidi ya mikopo yenye riba ndogo ya kila mwezi. Amefafanua kuwa benki za biashara hutoa mikopo kwa matarajio ya kurejesha ili kuzalisha faida, lakini TADB inajikita katika kutoa mikopo ili kutathmini na kusaidia maendeleo ya miradi.