Zanzibar yasajili miradi 300 ya uwekezaji ndani ya miaka mitatu
2023-11-01 22:43:51| cri

Mkurugenzi wa Maeneo Huria ya Uchumi kwenye Mamlaka ya Kuvutia Uwekezaji ya Zanzibar (ZIPA), Bibi Halima Wagao, amesema serikali ya Zanzibar imesajili uwekezaji wa moja kwa moja wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 4.5 katika kipindi cha miaka mitatu.

Akiongea jana mjini Zanzibar Bibi Wagao amesema miradi ya uwekezaji katika sekta ya utalii imezalisha ajira zipatazo 18,900 kwa vijana, na miradi mingine iliyozalisha ajira ni sekta ya mali zisizohamishika.

Bibi Wagao amesema ilichukua kipindi cha miaka sita kusajili kiasi sawa na kilichosajiliwa na Rais Mwinyi katika miaka mitatu.

Wawekezaji kwenye sekta ya mali zisizohamishika walitiwa moyo na ukweli kwamba serikali ilipitisha sheria inayowapa vibali maalum vya ukazi wale wanaojenga au kununua nyumba.