Sekta ya benki ya Rwanda yapata faida ya zaidi ya faranga bilioni 96 katika nusu ya kwanza ya 2023
2023-11-02 23:00:05| cri

Sekta ya benki nchini Rwanda imepata faida ya Faranga bilioni 96.9 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, zikiwa zimeongezeka kutoka bilioni 74.7 za mwaka 2022.

Benki kuu ya Rwanda imesema katika kipindi kama hicho mwaka 2021, sekta hiyo ilipata faida ya Faranga bilioni 55.9. Haya yameelezwa katika ripoti ya kila mwaka ya benki kuu ya 2022-2023, iliyotolewa Oktoba 30, ambayo inaelezea utendaji wa kifedha na uchumi mkuu wa nchi.

Sekta ya benki inayoundwa na taasisi 15 za benki za biashara, benki ndogo, benki za maendeleo na benki za ushirika, ilikuwa na raslimali zenye thamani ya Faranga bilioni 6.485 kwa Juni 2023, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 18.1 kutoka Faranga bilioni 5.492 kwa Juni 2022. 

Kwa upande mwingine, benki zilidumisha uwiano wa utoshelevu wa mtaji (CAR) wa asilimia 21.1, ukiwa ni zaidi ya kiwango cha chini cha udhibiti cha asilimia 15.