Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China inazitaka pande husika hasa Israel zijizuie, kutekeleza kihalisi azimio lililopitishwa tarehe 27 mwezi Oktoba na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kusitisha mapambano, kulinda raia, na kufungua njia ya msaada wa kibinadamu, ili kuepusha maafa makubwa zaidi ya kibinadamu.
Bw. Wang amesema, China imesikitishwa sana na idadi kubwa ya vifo vya raia wengi vilivyosababishwa na mashambulizi dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Ukanda wa Gaza, na kulaani vitendo hivyo.