Taasisi ya pili ya Confucius yafunguliwa nchini Botswana
2023-11-02 08:21:25| CRI

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia cha Botswana (BIUST) kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Yanshan (YSU) cha China, kimezindua Taasisi ya pili ya Confucius Jamanne huko Palapye katika Wilaya ya Kati nchini humo. 

Naibu mkuu wa Chuo hicho Otlogetswe Totolo akizungumza katika sherehe ya uzinduzi amesema, kwa kuwa China imepiga hatua kubwa katika sayansi, uhandisi na teknolojia, kujua lugha na utamaduni wa China kutaboresha uwezo wa wanafunzi kutafuta elimu ya juu zaidi nchini China, na kwamba wanafunzi wengi wa uhandisi na mazingira wa Chuo hicho wamenufaishwa na kujua lugha na utamaduni wa China, na kupata ajira katika sekta ya ujenzi.

Kwa upande wake rais wa YSU Zhao Dingxuan amesema Taasisi hiyo mpya ya Confucius itakusanya kikamilifu sifa za vyuo hivyo viwili, kutoa mafunzo ya Ufundi Stadi wa Kichina, kukuza kikamilifu elimu ya kimataifa ya lugha ya kichina, na kujenga daraja la kubadilishana na kujifunza kwa pamoja kati ya pande hizo mbili.