Duru mpya ya mgogoro kati ya Palestina na Israel yasababisha Wapalestina 8932 kuuawa
2023-11-02 10:47:51| cri

Gazeti la Palestina Al Quds limenukuu taarifa kutoka mamlaka ya afya ya eneo la Gaza likisema tangu mgogoro kati ya Palestina na Israel ulipuke tarehe 7 mwezi uliopita, idadi ya vifo vya Wapalestina katika eneo la Gaza imeongezeka hadi 8,805, wakiwemo watoto 3,648.

Akizungumzia shambulio la anga la Israel dhidi ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi katika ukanda wa Gaza ya Jabaliya, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu Bw. Martin Griffiths, amesema huu ni ukatili unaofanywa dhidi ya watu wa Gaza na mapigano katika ukanda wa Gaza yamezidi kuingia kwenye kipindi cha kutisha ambayo yatasababisha janga kubwa zaidi la kibinadamu, huku akitoa wito kwa nchi mbalimbali duniani kuchukua hatua kubadilisha hali hiyo.