Mkutano wa kwanza wa kazi ya fedha wa Kamati Kuu ya CPC wasisitiza maendeleo yenye ubora ya sekta ya fedha ya China
2023-11-02 14:00:26| cri

Tarehe 30 hadi 31 Oktoba, mkutano wa kwanza wa kazi ya fedha wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulifanyika nchini China, ambapo rais Xi Jinping wa China alihudhuria na kuhutubia mkutano, akifanya majumuisho kwa kazi za fedha katika miaka kumi iliyopita, na kupanga kazi za fedha kwa sasa na kwa kipindi kifuatacho. Mambo ya fedha ni damu ya uchumi wa taifa, pia ni sehemu muhimu ya nguvu kuu ya ushindani ya nchi. Ili kuimarisha uongozi mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kuhusu kazi za fedha, China iliunda Kamati ya Fedha ya Kamati Kuu ya CPC na Kamati ya Kazi ya Fedha ya Kamati Kuu ya CPC mwezi Machi mwaka huu, kamati ambazo zinashughulikia mpango na uratibu wa jumla juu ya utulivu na maendeleo ya sekta ya fedha.

Katika Fikra ya Xi Jinping Kuhusu Uchumi, fedha ni moja ya mambo makuu. Kwenye mkutano huo, Xi Jinping alikabiliana na suala lililopo kwa sasa na kusema, “hali ya ubora na ufanisi katika huduma ya fedha kwa uchumi halisi bado iko chini”. Uhusiano kati ya uchumi na fedha ni wa kuchangamana na kuathiriana. Uchumi halisi ni msingi wa maendeleo ya kifedha, bila ya uchumi halisi mzuri, maendeleo ya kifedha yatakuwa kama maji yasiyo na chanzo na mti usio na mzizi. Hivyo Xi Jinping alisisitiza kuwa fedha zinapaswa kutoa huduma yenye ubora kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Inapaswa kuimarisha huduma ya fedha yenye ubora kwa mkakati mkubwa, sekta muhimu na sehemu yenye udhaifu; Kufanya rasilimali nyingi za fedha zifanye kazi katika kuhimiza uvumbuzi wa teknolojia na sayansi, utengenezaji wa ngazi ya juu, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi na mashirika madogo na ya ukubwa wa kati, kuunga mkono zaidi utekelezaji wa mkakati wa maendeleo yanayochochewa kwa uvumbuzi na mkakati wa maendeleo yenye uwiano wa kikanda, na kuhakikisha usalama wa chakula na nishati; Inapaswa kuhamasisha rasilimali za fedha zinazotumiwa kwa ufanisi mdogo, kufanya vizuri kazi za kifedha kwenye nyanja tano yaani huduma za kifedha zinazokumbatia sayansi na teknolojia, zinazotumia mbinu za kijani, zinazonufaisha wote, zinazohusisha pensheni kwa wazee, na zinazotolewa kwa njia ya kidijitali; Kujitahidi kuweka taasisi za kisasa za kifedha na mfumo wa kisasa wa soko la kifedha, kuondoa vizuizi vinavyozuia fedha kuingia katika uchumi halisi; Inapaswa kuunga mkono mashirika makubwa ya kifedha yanayomilikiwa na serikali kuboresha huduma zao na kujitokeza kwenye sekta, na hatimaye kuwa nguvu kuu ya kuhudumia uchumi halisi na mwamba wa msingi thabiti unaohakikisha utulivu wa kifedha.

Kuhakikisha usalama wa kifedha ni ishara nyingine muhimu iliyotolewa kwenye mkutano huu. Mkutano huo umependekeza kwamba hivi sasa, migogoro na matatizo mbalimbali katika sekta ya fedha ya China yamechangamana, na bado kuna hatari nyingi za kiuchumi na kifedha. Ni lazima kuzingatia kwa kina kuimarisha usimamizi, kuzuia na kupunguza hatari, na kudumisha uthabiti wa sera ya kuzuia hatari za kifedha.

Mkutano huu pia umepanga ufunguaji mlango wa kiwango cha juu kwenye sekta ya fedha na kukuza biashara ya kimataifa ya soko la fedha la China. Mkutano huo umesisitiza kwamba inapaswa kutilia maanani "kuingiza" na vilevile "kuuza nje", kupanua kwa kasi ufunguaji wa kimfumo katika sekta ya fedha, na kuungana na kanuni za kimataifa za uchumi na biashara; kurahisisha uwekezaji na uwezeshaji wa kifedha wa kuvuka mipaka, na kuvutia taasisi nyingi zaidi za fedha za kigeni na mitaji ya muda mrefu kuendeleza biashara nchini China; kuimarisha ushindani na ushawishi wa Kituo cha Fedha cha Kimataifa cha Shanghai, kuimarisha na kuinua hadhi ya Hong Kong kama kituo cha fedha cha kimataifa, n.k.