Bolivia yatangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel
2023-11-02 08:27:44| cri

Serikali ya Bolivia imetangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel kwa kufuatia mashambulio ya Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Bolivia Bibi María Prada, amesema jumanne wiki hii, kwamba kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, serikali ya Bolivia imeamua kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel, pia inapanga kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa mapigano kati ya Palestina na Israel.