Wataalamu wakutana nchini Kenya kujadili njia za kuongeza kasi ya ukuaji wa kijani barani Afrika
2023-11-02 08:23:39| CRI

Mkutano wa Biashara ya Mabadiliko ya Tabianchi umeanza jana jijini Nairobi, Kenya, ambapo washiriki watajadili njia za kupata ufadhili wa fedha unaotakiwa ili kuongeza kasi ya mageuzi jumuishi ya Afrika kuhusu ukuaji wa kijani.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Kanda ya Mashariki mwa Afrika (IFC), Bi. Mary Porter Peschka amesema, Afrika inahitaji dola bilioni 190 za kimarekani kwa mwaka kati ya sasa na mwaka 2030 ili kutekeleza hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na dola nyingine bilioni 50 za kimarekani kwa mwaka itakapofika mwaka 2050 ili kufadhili hatua hizo.

Mkuu wa Idara ya Mazingira, jamii na Uongozi Endelevu katika Benki Kuu ya Ghana, Ignatius Wilson, amesema nchi hiyo kwa sasa inaandaa miongozo itakayoshawishi sekta binafsi kuwekeza katika miradi itakayopunguza utoaji wa hewa chafu nchini humo.