Mashirika ya UM yatoa wito wa kusitisha mara moja mapambano kati ya Palestina na Israel
2023-11-03 11:06:15| cri

Timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya umoja huo wameonya kuwa mfumo wa kibinadamu wa ukanda wa Gaza unaporomoka, huku wakitoa wito wa kusitishwa vita mara moja, ili kuhakikisha vifaa vya msaada vinaingia katika ukanda wa Gaza kwa wakati.

Timu ya wataalamu inayoundwa na waandaaji saba maalumu wa ripoti wa UM tarehe 2 Novemba ilitoa taarifa mjini Geneva ikisema, njia ya kusafirisha vifaa vya msaada kwenda Gaza imezuiliwa tangu duru hii ya mapambano kati ya Palestina na Israel ilipolipuka.

Wakati huohuo Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito tena kutimiza usitishwaji vita wa kibinadamu mara moja, ili kuokoa maisha ya maelfu ya majeruhi na wagonjwa wenye matatizo sugu ya kiafya.