UM waongeza doria ya usalama nchini Sudan Kusini baada ya kutekwa kwa mfanyakazi wa msaada
2023-11-03 08:39:06| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan (UNMISS) imesema imeongeza doria za usalama katika eneo la Ulinzi wa Raia (PoC) mjini Malakal, mkoa wa Upper Nile, kaskazini mwa Sudan Kusini.

Hatua hiyo imekuja baada ya kutekwa nyara kwa Emmanuel Obayi, ofisa lishe anayefanya kazi na Kundi la Madaktari wa Kimataifa katika eneo hilo Oktoba 27.

Mkuu wa kitengo cha habari cha UNMISS Ben Malor amesema, tukio hilo limeripotiwa kwa uongozi wa Tume hiyo, na kusisitiza kuwa, UNMISS iko tayari kuchukua hatua za kumwokoa mfanyakazi huyo.