Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC akutana na makamu mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala la Sudan
2023-11-03 08:44:22| cri

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wang Yi, amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala la Sudan Bw. Malik Agar mjini Beijing hapo jana.

Bw. Wang amesema, China itaendelea kuiunga mkono Sudan katika kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi, kuiunga mkono nchi hiyo katika kufikia amani na utulivu wa ndani, na katika kutafuta njia ya maendeleo inayolingana na hali yake ya kitaifa.

Kwa upande wake, Bw. Malik Agar amesema, Sudan inatilia maanani sana umuhimu wa China katika mambo ya kimataifa, ameishukuru China kwa kutilia maanani hali ya Sudan, na anatarajia China kuiunga mkono Sudan ili kurejesha utulivu, ujenzi mpya na kupata maendeleo.