Tanzania, shirika la ushindani la EAC wasaini makubaliano ya kuhimiza biashara
2023-11-03 11:13:42| cri

Makubaliano ya kuhimiza biashara ya kuvuka mpaka kati ya Tume ya Ushindani wa Haki ya Tanzania (FCC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yamesainiwa ili kuhimiza biashara kati ya Tanzania na jumuiya hiyo.

Kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo wito wa kuhimiza biashara ya kuvuka mpaka katika nchi za Afrika Mashariki ulitolewa, na kutaka makubaliano hayo pia kuendeleza sera na sheria ya ushindani.

Msajili wa Mamlaka ya Ushindani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCA) Bibi Lilian Mukoronia amesema makubaliano hayo yanapaswa kufanya kazi kwa njia ya kuwezesha biashara ya mipakani katika eneo la Afrika Mashariki na mamlaka hiyo inajadiliana na nchi washirika ili kuendeleza sera na sheria ya ushindani ili kurahisisha biashara ya kikanda.

Bibi Mukoronia ameipongeza FCC kwa kuwa na hamasa katika mpango huo, akisema hatua hiyo inatakiwa kuunga mkono mkakati wa kikanda wa kutengeneza soko la pamoja lenye ushindani.