Waziri mkuu wa DRC azindua kituo cha data kilichojengwa na Kampuni ya Huawei ya China
2023-11-03 08:37:42| CRI

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Sama Lukonde Kyenge amezindua kituo cha data katika Wizara ya Fedha ambacho kimejengwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya Huawei ya China.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Bw. Kyenge amesema ujenzi huo unaonesha ushirikiano kati ya DRC na China kwa kuwa kituo hicho kitaonesha umuhimu mkubwa katika maendeleo ya kijamii nchini DRC.

Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Bw. Nicolas Kazadi amesema kituo hicho kitakuza mambo ya kisasa, utawala bora, na kampeni ya kupambana na ufisadi nchini humo.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini DRC Bw. Zhao Bin amekitaja kituo hicho kama “Mafanikio makubwa ya ushirikiano kati ya China na DRC” katika sekta ya habari za dijitali, na kusema kituo hicho kitaiwezesha DRC kuharakisha ushirikiano wake katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya kimataifa, na kuleta msukumo mpya katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya DRC.