Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yasema Sudan inakabiliwa na janga kubwa la kibindamu
2023-11-03 10:58:16| cri

Ripoti iliyotolewa jana na ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Sudan inakabiliana na janga kubwa la kibinadamu lisilo na kifani tangu mgogoro ulipuke nchini humo, ambapo nusu ya watu wake wakiwemo watoto milioni 14 wanahitaji msaada wa kibinadamu, na watu milioni 20.3 wanakumbwa na ukosefu wa usalama wa chakula. Licha ya hayo, Sudan inakabiliana na hatari ya maambukizi makubwa ya magonjwa mbalimbali kama vile kipindupindu, homa ya dengue, surua na malaria.

Ripoti hiyo pia imesema mipango ya utoaji wa msaada wa kibinadamu inakabiliana na ukosefu wa fedha. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Sudan zinahitaji dola za kimarekani bilioni 2.6, lakini sasa asilimia 33 tu ya fedha hizo zimepatikana.