ATMIS na jeshi la Somalia zaongeza mapambano dhidi ya kundi la al-Shabaab
2023-11-03 08:39:40| CRI

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema imeongeza operesheni za pamoja za kijeshi na jeshi la Somalia, licha ya kusitishwa kwa miezi mitatu ili kuwezesha awamu ya pili ya kupunguza askari wake kufanyika.

Kamanda wa ATMIS Sam Okiding amesema, baada kusitishwa huko kutokana na ombi la Somalia, Tume hiyo imepanga upya askari wake na inaendelea na mapambano dhihi ya kundi la al-Shabaab.

Kwa mujibu wa mipango ya usalama ya Somalia, ATMIS itaondoa askari wake kwa awamu katika miezi 14 ijayo, kabla ya kuondoka rasmi mwishoni mwa mwaka 2024, na jeshi la Somalia kuchukua wajibu wa usalama.