Ethiopia yapongeza kumbukumbu ya kwanza ya makubaliano ya amani yaliyomaliza vita ya miaka miwili
2023-11-03 08:38:22| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, Meles Alem, amepongeza kumbukumbu ya kwanza ya makubaliano ya amani yaliyomaliza vita iliyodumu kwa miaka miwili katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Akizungumza na wanahabari hapo jana, Alem amesema makubaliano ya amani ya Pretoria yaliyosainiwa mwaka mmoja uliopita na serikali ya Ethiopia na Kikosi cha Harakati za Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) yamaimarisha msimamo wa kimataifa wa nchi hiyo.

Amesema makubaliano ya amani ya Pretoria yameimarisha diplomasia ya Ethiopia na kuboresha uhusiano wake na nchi na mashirika ya kimataifa, huku mfano bora ukiwa ni kufanikiwa kwa nchi hiyo kuwa nchi mwanachama wa BRICS.

Novemba 2, 2022, serikali ya Ethiopia na TPLF zilisaini makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mjini Pretoria, Afrika Kusini, na hivyo kumaliza vita iliyodumu kwa miaka miwili.