Kituo cha ufuatiliaji wa ugonjwa wa Kichocho kilichojengwa kwa msaada wa China chaanzishwa Zanzibar
2023-11-03 08:38:21| cri

 

Hafla ya uzinduzi wa Kituo cha ufuatiliaji wa ugonjwa wa Kichocho kilichojengwa kwa msaada wa China imefanyika jumatano wiki hii visiwani Zanzibar, Tanzania, na kuhudhuriwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar Nassor Mazrui na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Zhang Zhisheng.

Bw. Mazrui amesema, kukinga na kudhibiti ugonjwa wa Kichocho ni kazi ngumu ya majukumu ya afya ya umma ya Zanzibar, na chini ya msaada wa wataalamu wa China, kazi hiyo imepata mafanikio makubwa. Pia ameishukuru serikali ya China kwa kutuma tena kikundi cha wataalamu kwenye Zanzibar.