WMO latoa ripoti ya kila mwaka inayochambua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa afya ya binadamu
2023-11-04 22:56:09| cri

Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetoa ripoti ya mwaka 2023 kuhusu huduma za hali ya hewa, ambayo imezingatia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa afya ya binadamu. Katika mkutano na waandishi wa habari, wataalam wamesema kutokana na ongezeko la joto duniani kupita viwango vya rekodi, afya ya binadamu inastahili kuzingatiwa. Mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kurudisha nyuma maendeleo ya miongo kadhaa katika kuboresha afya na ustawi, na makundi ya kijamii yaliyo hatarini kuathirika zaidi. Ripoti hiyo inaangazia mahitaji ya habari na huduma zinazolengwa za hali ya hewa ili kusaidia sekta ya afya katika kukabiliana na hali mbaya ya hewa, mabadiliko ya magonjwa ya kuambukiza, na wasiwasi wa usalama wa chakula na maji.

Katibu Mkuu wa WMO Prof. Petteri Taalas amesema karibu dunia nzima imekumbwa na wimbi la joto mwaka huu, na kuanza kwa hali ya El Nino mwaka huu kunaongeza sana uwezekano wa kuvunja rekodi za joto. Ameongeza kuwa katika maeneo mengi ya ardhi ya dunia na maeneo ya bahari yamekumbwa na joto kali, na kusababisha changamoto kubwa za tabianchi. Amesisitiza kuwa kwa kuongoza uwekezaji na kukuza ushirikiano, na kwa kuboresha uwezo wa sayansi ya hali ya hewa na huduma, itakuwa na athari kubwa katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.