Rais Xi Jinping wa China aandika barua kwa Maonesho ya sita ya CIIE
2023-11-05 14:16:39| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ameandika barua kwa Maonesho ya sita ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya Chin CIIE.

Rais Xi amesema, tangu mwaka 2018, China imefanikiwa kufanya awamu 5 ya maonyesho ya CIIE. Maonesho hayo yametumia ubora wa soko kubwa la China, kuonesha umuhimu wake katika uagizaji wa kimataifa, uwekezaji, mawasiliano ya utamaduni na watu, ufunguaji mlango na ushirikiano, na kutoa mchango kwa kuharakisha ujenzi wa muundo mpya wa maendeleo na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia.

 

Maonyesho ya sita ya CIIE yamefunguliwa leo mjini Shanghai.