Aliyekuwa kiongozi wa serikali ya kijeshi ya Guinea arudishwa jela
2023-11-06 08:39:15| CRI

Mnadhimu mkuu wa Jeshi la Serikali ya Mpito ya Guinea Bw. Ibrahima Sory Bangoura alitoa taarifa mchana wa tarehe 4, na kusema kiongozi wa zamani wa serikali ya kijeshi ya Guinea aliyetoroka gerezani mapema asubuhi hiyo Moussa Dadis Camara amerudishwa tena jela.

Taarifa hiyo imesema wanajeshi wa serikali ya mpito wamemrudisha Camala na maofisa wengine wawili wa zamani wa jeshi katika gereza la Kalum wilaya ya Conakry. Watatu hao kwa sasa wako salama.

Katika taarifa hiyo, Bw. Bangoura alitoa wito kwa watu wa Guinea kurejea katika maisha ya kawaida.

Tarehe 4 saa 5 asubuhi kwa saa za huko, kundi la watu wasiojulikana wenye silaha walivamia gereza la Wilaya ya Calume na kumsaidia Camara na maofisa wengine wawili wa zamani wa serikali ya kijeshi ya Guinea kutoroka. Wanajeshi wa serikali ya mpito ya Guinea mara moja walifunga barabara inayoelekea wilaya ya Calume.