Maonyesho ya CIIE ya China yatambuliwa kimataifa kwa kukuza maendeleo na ushirikiano
2023-11-06 08:15:03| CRI

Maonesho ya sita ya Uagizaji wa Kimataifa ya China (CIIE), yaliyoanza hapa Jumapili yamepongezwa na viongozi na maofisa wa nchi mbalimbali kwa mchango wake wa kutoa fursa za biashara kwa makampuni ya kimataifa, kuhimiza biashara na ushirikiano wa kimataifa, na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi duniani.

Waziri Mkuu wa Australia Bw. Anthony Albanese amesema Australia na China zimenufaika kutokana na maendeleo na utulivu wa kikanda, na kuwa biashara ya bidhaa na huduma kati ya pande mbili imeongezeka karibu maradufu tangu Mkataba wa Biashara Huria kati ya China na Australia ulipoanza kutekelezwa mwaka 2015.

Waziri Mkuu wa Cuba Bw. Manuel Marrero Cruz amesema Cuba inatilia maanani sana na inashiriki mara kwa mara katika maonesho hayo muhimu, na kusema kufanyika kwa maonesho hayo kutasaidia jumuiya ya kimataifa kuhimiza ufufuaji wa uchumi wa dunia na maendeleo ya biashara.

Viongozi wengine kutoka Kazakhstan, Serbia, Afrika Kusini na Iran pia wameyapongeza maonesho hayo.