Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa mkutano wa kwanza wa BRI kuhusu mabadilishano ya sayansi na teknolojia
2023-11-06 14:33:57| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa mkutano wa kwanza wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kuhusu Mabadilishano ya Sayansi na Teknolojia uliofanyika mjini Chongqing, kusini magharibi mwa China jumatatu wiki hii.

Katika barua yake, rais Xi amesema Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ulifanyika kwa mafanikio, na kuashiria ngazi mpya ya maendeleo ya ubora wa juu ya Pendekezo hilo, na sayansi na teknolojia ni sehemu muhimu.

Amesema China iko tayari kushirikiana na nchi nyingine kunufaika na fursa za ukuaji wa uvumbuzi, kufungua fursa za ushirikiano wa uvumbuzi, kuimarisha uhusiano wa uvumbuzi, na kuhimiza mafanikio ya uvumbuzi ili kufaidisha watu wa nchi zote, na hivyo kutoa mchango katika maendeleo ya ubora wa juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na katika ujenzi wa jamii ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.