Uganda, Vitol Bahrain waichagua bandari ya Dar es Salaam, Tanzania, kuingiza mafuta
2023-11-06 14:32:03| cri

Serikali ya Uganda na kampuni ya Vitol Bahrain E.C wamechagua bandari ya Dar es Salaam, nchini Tanzania, kuingizia mafuta, ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kukuza uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo.

Uamuzi huo umefikiwa siku chache baada ya kampuni ya Vitol E.C kupata kibali cha kusambaza mafuta nchini Uganda kilichotolewa na Kampuni mpya ya Mafuta iliyoundwa na serikali ya Uganda ili kusimamia uingizaji na usambazaji wa mafuta.

Waziri wa Madini na Nishati wa Uganda, Dk. Nankabirwa Sentamu amesema, Kampuni ya Vitol E.C imeahidi kusaidia gharama za ujenzi wa kituo cha ziada cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Namwambula nchini Uganda.