Raia 20 wauawa kufuatia pande hasimu za Sudan kufyatuliana mizinga magharibi mwa Khartoum
2023-11-07 08:10:09| CRI

Shirikisho la Wanasheria la Sudan limesema, tukio la kufyatuliana mizinga kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) limesababisha vifo vya raia zaidi ya 20 kwenye eneo la Omdurman, magharibi mwa Khartoum.

Shirikisho hilo lisilo la kiserikali limetoa taarifa ikizitaka pande zinazopambana kuepuka maeneo yenye watu wengi na kuwajibika kwa vifo na majeruhi ya raia. Pia shirikisho hilo limetoa wito kwa pande hasimu kusitisha mapigano na kutafuta suluhu ya amani.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kikosi cha RSF Novemba 5 kilishambulia ghala moja la silaha kwenye eneo la Omdurman, na jeshi la Sudan likatoa video ya kujibu shambulizi hilo kwenye mtandao wa kijamii.