Umoja wa Afrika watoa mwito wa uwekezaji katika elimu na uendelezaji wa ustadi barani humo
2023-11-07 14:52:50| cri

Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito wa uwekezaji zaidi katika elimu na uendelezaji wa ustadi barani humo kwa kutumia aina mpya ya makubaliano ya kijamii.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa imesema, wito huo umetolewa jana na Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia elimu, sayansi, teknolojia na uvumbuzi, Mohamed Belhocine, alipohutubia Mkutano wa Tano wa Kamati ya Sera za Jamii, Umasikini na Jinsia uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Bw. Belhocine amesisitiza kuwa makubaliano mapya ya kijamii yanaozingatia elimu na uendelezaji wa ustadi ni ufunguo wa kuonyesha uwezo wa Afrika na kutimiza matarajio ya watu wake.