China na Australia zaanza njia sahihi ya kuboresha uhusiano
2023-11-07 14:43:56| cri

Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese mjini Beijing jana jumatatu.

Katika mazungumzo yao, rais Xi amesema China na Australia zimeanza njia sahihi ya kuboresha uhusiano. Amesema nchi hizo mbili zote ni nchi za Asia na Pasifiki na wanachama muhimu wa Kundi la Nchi 20 (G20), na kwamba zinaweza kuwa wenzi wa kuaminiana na kunufaishana mafanikio ya pamoja.

Rais Xi ameongeza kuwa, China na Australia zinapaswa kufuata mwelekeo wa nyakati, kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaohusisha kutendeana kwa usawa, kutafuta maoni ya pamoja na kuweka pembeni tofauti na ushirikiano wa kunufaishana, na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati yao.

Bw. Albanese amesema kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuheshimianana, kunufaishana kwa usawa, kudumisha mawasiliano, kuimarisha maelewano na ushirikiano, na kutimiza hali ya kunufaishana. Amesema kwa kuwa Australia na China zina mifumo tofauti ya kisiasa, ni kawaida kuwa na maoni tofauti, lakini hazitakiwi kuathiri mwelekeo wa uhusiano. Ameongeza kuwa, Australia na China zina maslahi mengi ya pamoja, mazungumzo na ushirikiano ni chaguo sahihi.