Serikali ya Ethiopia yasisitiza dhamira yake katika kutekeleza makubaliano ya amani
2023-11-07 08:15:56| CRI

Serikali ya Ethiopia imesema makubaliano ya amani ambayo yalimaliza mgogoro uliodumu kwa miaka miwili, na kuchangia hali ya maisha katika eneo lililoathiriwa la kaskazini mwa nchi hiyo kurudi kuwa ya kawaida.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imesema serikali imeonesha dhamira yake thabiti katika utekelezaji wa makubaliano hayo kupitia hatua madhubuti za kujenga uaminifu na kuimarisha amani.

Mwezi Novemba 2022, serikali ya Ethiopia na Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray (TPLF) walisaini makubaliano ya kusimamisha uhasama mjini Pretoria, ili kumaliza mgogoro wa miaka miwili.

Serikali ya Ethiopia imesema imechukua hatua kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kukomesha operesheni zote za kijeshi na kauli za chuki dhidi ya kundi la TPLF, kuharakisha na kuwezesha utoaji wa msaada wa kibinadamu, na kuwezesha kurejesha huduma zote muhimu katika eneo la Tigray.