Tanzania yaongeza bajeti yake kwa mwaka mpya wa fedha
2023-11-07 14:48:54| cri

Serikali ya Tanzania imetangaza mapendekezo ya bajeti ya taifa ya shilingi trilioni 47.42, sawa na dola za kimarekani bilioni 18.94, katika mwaka mpya wa fedha utakaoanzia Julai 1, mwaka 2024 na kumalizika Juni 30, mwaka 2025.

Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Mwigulu Nchemba amewasilisha mapendekezo hayo katika Bunge la nchi hiyo, na kusema bajeti hiyo inazidi ile ya mwaka uliopita wa fedha kwa trilioni tatu, na kwamba shilingi trilioni 34.43 zitakusanywa kutoka vyanzo vya ndani ambavyo ni sawa na asilimia 72.6 ya bajeti ya jumla huku wenzi wa maendeleo wakitarajiwa kuchangia shilingi trilioni 4.29.

Pia ameongeza kuwa serikali ya Tanzania inatarajia kukopa shilingi trilioni 6.14 kutoka ndani, na shilingi trilioni 2.55 zitapatikana kutoka kwa wakopeshaji wa kigeni.