Rais wa China asisitiza kujenga China ya kupendeza
2023-11-08 13:54:06| cri

Rais Xi Jinping wa China Jumatano alihimiza juhudi za kujenga China ya kupendeza kwa pande zote na kuboresha mfumo wa usimamizi wa sekta ya kuhodhi mitandao ya asili.

Rais Xi amesema hayo jana alipoendesha mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Kuimarisha Mageuzi kwa Pande Zote. Miongozo mbalimbali ilipitishwa kwenye mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kuhimiza ujenzi wa China ya kupendeza kwa pande zote, kuboresha zaidi mfumo wa bajeti ya matumizi ya mitaji ya taifa, kuboresha mfumo wa usimamizi wa sekta ya kuhodhi mitandao ya asili, kuimarisha zaidi usimamizi wa wataalamu wanaoshiriki katika kufanya maamuzi ya umma, na kuimarisha usimamizi na udhibiti wa eneo maalumu kwa mazingira ya kiikolojia.

Pia rais Xi amesema ujenzi wa China ya kupendeza ni kazi muhimu katika kuijenga China kwa pande zote kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa, na kuhimiza juhudi za kutimiza lengo la kujenga China ya kupendeza itakapofika mwaka 2035.