Wizara ya Elimu nchini Tanzania kuimarisha Tehama
2023-11-08 22:52:54| cri

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Ofisi ya Elimu ya Mji wa Gwangju nchini Korea Kusini (GMOE) zimesaini hati ya makubalino ya miaka minne katika mradi wa kuimarisha matumizi ya TEHAMA nchini humo.

Hati hizo zimesainiwa jana jumanne jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TET, Dk Anneth Komba amesema, makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na Ofisi ya Elimu ya Gwangju kuipatia Taasisi ya Elimu kompyuta na vifaa vingine vya TEHAMA kila mwaka, na TET itawajibika kulipia gharama za kuvikomboa vifaa hivyo bandarini pamoja na gharama ya kuvisafirisha katika shule husika.