Waziri Mkuu wa China atuma salamu za pongezi kwa waziri mkuu mpya wa Cote d’ivore
2023-11-08 08:37:21| CRI

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang ametoa pongezi kwa Bw. Robert Beugre Mambe kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu wa Cote d’ivore .

Bw. Li Qiang amesema China na Cote d’ivore ni marafiki na washirika wazuri. Huu ni mwaka wa 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na hivi sasa uhusiano kati ya China na Cote d’ivore unaendelea vizuri, na kiwango cha kuaminiana kisiasa kimeendelea kuongezeka siku hadi siku, na pande hizo mbili zimepata mafanikio makubwa katika ujenzi wa pamoja wa pendekezo la Ukanda moja, Njia moja. Amesema China inapenda kushirikiana na Cote d’ivore katika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili na kuhimiza ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili uendelee kupata mafanikio mapya.