Rais wa China atoa wito wa kufanya mtandao kunufaisha watu wote duniani
2023-11-08 16:00:56| cri

Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kuufanya mtandao wa internet kunufaisha watu wa nchi zote.

Rais Xi amesema hayo jumatano alipohutubia kwa njia ya video ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka 2023 wa Mtandao Duniani (WIC) unaofanyika Wuzhen nchini China.

Rais Xi amesema lengo la kujenga kwa pamoja jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja katika mtandao, ambalo alilipendekeza katika mkutano wa pili wa WIC mwaka 2015, limetambuliwa kimataifa na kupokelewa vizuri.

Amesema lengo hilo limejibu maswali ya zama hizi yanayohusiana na maendeleo duni, kukabiliana na changamoto za kiusalama, na kuimarisha kufundishana kati ya staarabu tofauti.