Pande zinazopambana nchini Sudan zashutumiana kuhusika na mlipuko dhidi ya kiwanda cha kusafisha mafuta
2023-11-08 08:16:18| CRI

Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) wameshutumiana kuhusika na mlipuko uliotokea katika kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta mapema ya jana.

Jeshi la Sudan limetoa taarifa likisema RSF ilipeleka boza kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta na kulijaza mafuta bila kufuata taratibu za usalama, na kusababisha mlipuko katika Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Khartoum.

RSF imelishutumu jeshi la Sudan kwa kutuma ndege yake ya kivita "kushambulia uwezo uliobaki wa wasudan na miundombinu ya nchi," na kuongeza kuwa shambulio la bomu ni "uhalifu wa kivita."

Mapambano makali kati ya pande hizo mbili yameendelea mjini Khartoum na maeneo mengine tangu Aprili 15, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000.