Wataalamu wa China na Rwanda watafuta njia za usimamizi endelevu wa maliasili
2023-11-09 08:05:47| CRI

Wasomi na wataalamu kutoka China na Rwanda waliokutana jana kwenye kongamano moja la kimataifa kuhusu mazingira, wamesema athari zinazoongezeka za mabadiliko ya tabianchi zinahitaji ushirikiano wa kuhakikisha usimamizi uendelevu wa maliasili.

Mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu Mazingira, Nishati na Maendeleo uliofanyika jana mjini Kigali, Rwanda uliandaliwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Lay Adventists cha Kigali, Kituo cha Utafiti wa Pamoja kati ya China na Afrika cha Akademia ya Sayansi ya China (CAS), Taasisi ya Ikolojia na Jiografia ya Xinjiang ya CAS, chini ya kaulimbinu ya “Usimamizi Endelevu wa Maliasili”.

Akifungua mkutano huo, balozi wa China nchini Rwanda Wang Xuekun amesema, ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia ni moja ya nyanja tano za maendeleo ya China, na pia ni hatua muhimu kwenye njia ya China kujijenga kuwa nchi ya kisasa.