China kufanya kila juhudi kulinda raia, kutuliza mgogoro, na kuanzisha tena mazungumzo ya amani
2023-11-09 08:36:55| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana amesema China ikiwa ni mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na nchi mwanachama inayowajibika katika jumuiya ya kimataifa, itaendelea kufanya mawasiliano na pande husika na kufanya juhudi zote kulinda raia, kutuliza mgogoro, kuanzisha upya mazungumzo ya amani, na kutimiza amani.

Bw. Wang Wenbin amesema China inaomboleza vifo vya watu wa Palestina na Israel waliopoteza maisha katika mgogoro huo, na kusema matumizi ya nguvu hayawezi kuleta usalama na amani ya kudumu. Kuwaachilia mateka, kulinda usalama wa raia na vifaa vya kiraia, kufungua njia za misaada ya kibinadamu, na kuanzisha tena mazungumzo ni jukumu la pande husika na pia ni madhumuni ambayo jumuiya ya kimataifa inapaswa kujitahidi kufikia.