Baraza la Uwekezaji Afrika la mwaka 2023 lafunguliwa Morocco
2023-11-09 08:52:31| CRI

Shughuli za Siku za Soko za Baraza la Uwekezaji Afrika la mwaka 2023 zilimefunguliwa mjini Marrakech, Morocco.

Mfalme Mohammed VI wa Morocco amehutubia ufunguzi wa baraza hilo lenye kaulimbiu ya "Kuunda Minyororo ya Thamani ya Afrika", akisema Bara la Afrika "linakabiliwa na changamoto zenye utatanishi za kiuchumi zinazochochewa na mivutano ya siasa ya kijiografia nje ya Afrika," na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa viwango vya riba, na kuendelea kwa mfumuko wa bei pia kumeleta shinikizo kwa uchumi wa Afrika.

Mfalme huyu amesisitiza kuwa Morocco imekuwa ikitoa wito wa kuimarishwa kwa mifumo ya uratibu na ushirikiano baina ya nchi za Afrika, ikiwa na maono ya kufikia mafungamano ya kiuchumi ya kikanda. Pia alizitaka nchi za Afrika kuwekea kipaumbele katika maendeleo ya miundombinu.