Washiriki wa Kongamano la Abuja waona “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeiletea Afrika fedha na teknolojia zinazohitajika
2023-11-09 10:14:02| CRI

Karibu tena msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti inayohusu Washiriki wa Kongamano la Abuja waona “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeiletea Afrika fedha na teknolojia zinazohitajika, ikikumbukwa kwamba hivi karibuni mkutano wa tatu wa Ushirikiano wa Ukanda mmoja, Njia Moja ulimalizika hapa Beijing. Lakini pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi, na yatazungumzia wawakilishi wa vyuo vikuu 14 kutoka mkoa wa Hubei nchini China wametembelea Chuo Kikuu cha Nairobi wakati wa maonyesho maalum ya elimu ya juu.