China yatoa waraka kuhusu sera za CPC katika utawala wa Xizang katika zama mpya
2023-11-10 20:18:59| cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka kuhusu utawala wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika mkoa unaojiendesha wa Xizang katika zama mpya.

Waraka huo unaoitwa “Sera za CPC kuhusu Utawala wa Xizang katika Zama Mpya: Mtazamo na Mafanikio,” unasema miongozo ya CPC kwa ajili ya utawala wa Xizang katika zama mpya umeleta maendeleo ya pande zote na mafanikio ya kihistoria katika sekta mbalimbali mkoani humo.