Rais Xi Jinping wa China akagua kazi ya ukarabati baada ya maafa ya mafuriko mjini Beijing na mkoani Hebei
2023-11-10 21:32:26| cri

Tarehe 10 Novemba, Rais Xi Jinping wa China alipokagua kazi ya ukarabati baada ya maafa ya mafuriko mjini Beijing na mkoani Hebei, alisisitiza kwamba kamati za chama na serikali za ngazi mbalimbali na idara husika zinatakiwa kutekeleza kwa makini mipango ya Kamati Kuu ya Chama cha CPC na kushughulikia ukarabati baada ya maafa kwa makini, ili kuhakikisha maisha ya watu katika majira ya baridi. Serikali inatakiwa kutilia maanani maslahi ya watu, kuharakisha ujenzi wa miradi ya kuzuia mafuriko, na kuinua uwezo wa kupunguza maafa na kufanya uokoaji.