Mkutano wa Kilele wa Uwekezaji Endelevu kati ya China na Afrika wafanyika Nairobi
2023-11-10 08:17:13| CRI

Mkutano wa Kilele wa Uwekezaji Endelevu kati ya China na Afrika ulifanyika jana Alhamisi mjini Nairobi, Kenya, ambapo washiriki wamerejea wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano ili kuhakikisha mpito wa haki na kijani.

Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF), Muungano wa Biashara za China Barani Afrika Kwa Wajibu wa Kijamii (ACBASR) na Kituo cha Kifedha cha Ushirikiano wa Kusini-Kusini, umehudhuriwa na watunga sera, wanadiplomasia, wawekezaji na wajasiriamali.

Wajumbe walioshiriki kwenye mkutano huo wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano ili kuhimiza mpito wa nishati ya kijani kupitia mpango kabambe wa kifedha, maendeleo ya ufundi stadi na matumizi ya teknolojia.