UM watoa fedha kuisaidia Somalia kukabiliana na mafuriko
2023-11-10 08:58:33| CRI

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetenga dola milioni 25 za Kimarekani kuisaidia Somalia kukabiliana na mafuriko ambayo yameathiri karibu watu milioni 1.2.

OCHA imesema fedha hizo zitatumiwa kuokoa maisha ya watu, kuzuia milipuko ya magonjwa, na kukabiliana na uhaba wa chakula.

OCHA inakadiria kuwa katika msimu wa mvua ulioanza mwezi Oktoba hadi Disemba, mafuriko yanaweza kuathiri watu milioni 1.6, na kuharibu hekta milioni 1.5 za mashamba. Imetahadharisha kuwa mafuriko hayo hayakushuhudiwa katika miaka 100 iliyopita nchini Somalia, na yanakadiriwa kuleta athari kubwa za kibinadamu.