Wasomi wa China na Zimbabwe waeleza nia ya kutekeleza kwa pamoja Pendekezo la Usalama Duniani na kulinda utulivu barani Afrika
2023-11-10 08:45:44| CRI

Semina ya “Hali ya usalama barani Afrika na Maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika” imefanyika tarehe 8 mwezi huu mjini Harare Zimbabwe, ambayo imeshirikisha wasomi wa China na Zimbabwe zaidi ya 30 kutoka jumuiya za washauri bingwa kwenye nyanja za amani, usalama na upokonyaji silaha.

Wasomi waliohudhuria semina hiyo wamekubali kuwa Pendekezo la Usalama Duniani(GSI)lililotolewa na China linafaa kwa mahitaji halisi ya usalama na maendeleo barani Afrika, na wanapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano husika kati ya China na Zimbabwe na kulinda usalama na utulivu wa Afrika kwa pamoja.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Watu wa China kwa ajili ya Amani na Upokonyaji Silaha Bw. An Yuejun alipohutubia semina hiyo alisema ushirikiano na Afrika katika sekta ya usalama ni moja ya maelekezo muhimu ya pendekezo hilo, na shirikisho hilo linaiunga mkono Afrika kutatua masuala yake kwa njia ya kiafrika na linapenda kutoa mchango katika kutekeleza pendekezo hilo na kulinda utulivu wa Afrika likishirikiana na wasomi na mashirika husika ya Zimbabwe.